Afisa Maendeleo ya Jamii aliyepongezwa na Waziri Bashungwa apewa tuzo na Milioni 3/-

NA DIRAMAKINI

HALMASHAURI ya Manispaa ya Tabora mkoani Tabora imeungana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhe. Innocent Bashungwa kumpongeza Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Tabora Bi. Tumaini Mgaya kwa uongozi wake mahiri wa kuisimamia Idara ya Maendeleo ya Jamii.
Manispaa ya Tabora wamefanya hivyo ikiwa ni siki chache baada ya Mhe. Innocent Bashungwa kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora kumuandalia Tuzo Maalum ya kutambua mchango wake katika idara hiyo akisema amekua Afisa Maendeleo bora na wa mfano.
Bi. Mgaya amekabidhiwa tuzo hiyo pamoja na shilingi milioni tatu. Awali, Waziri Bashungwa alieleza kuwa, kufanya hivyo kutatoa motisha kwa wengine kufanya kazi kwa bidii, umoja na mshikamano lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Post a Comment

0 Comments