Ahmed Arajiga kutoka Manyara akabidhiwa jukumu la Simba na Yanga SC wiki hii

NA DIRAMAKINI

REFA Ahmed Arajiga wa Manyara ndiye atakayechezesha mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Arajiga atasaidiwa na Frank Komba wa Dar es Salaam na Mohamed Mkono wa Tanga, wakati refa wa akiba mezani atakuwa Heri Sasii wa Dar es Salaam.
Nusu Fainali nyingine ya Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya Azam FC na Coastal Union Jumapili Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha itachezeshwa na Ramadhani Kayoko Wa Dar es Salaam atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Soud Lila wa Dar es Salaam.
Kingilio cha chini katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya watani, Simba na Yanga ni Sh. 10,000 Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Taarifa ya TFF imesema viingilio vingine ni Sh, 30,000 VIP A na Sh, 20,000 VIP B na mchezo utaanza Saa 9:30 Alasiri.

Post a Comment

0 Comments