Rais Samia atembelea eneo la Makumbusho na kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah jijini Accra

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah wakati alipotembelea eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) katika Jiji la Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Mnara wa kumbukumbu katika eneo la Makaburi alipozikwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah wakati alipotembelea eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) katika Jiji la Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama mbele ya mnara wa kumbukumbu kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah katika eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) Jijini Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo wakati alipotembelea katika eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) Jijini Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA), Wamkele Mene katika Ofisi za AfCFTA Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkataba wa eneo huru la Biashara Barani Afrika (The African Continental Free Trade Area), katika Ofisi za (AfCFTA) Jiji la Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022. (PICHA NA IKULU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news