Balozi Sokoine ashiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu SADC

NA DIRAMAKINI

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika Mei 5,2022 kwa njia ya mtandao.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akishiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika Mei 5,2022 kwa njia ya mtandao katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akishiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo kwa njia ya mtandao katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agnes Kayola.

Balozi Sokoine ameshiriki mkutano huo akiwa katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC unaotarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao leo Mei 6, 2022.

Pamoja na masuala mengine, Makatibu Wakuu wamejadili athari za mafuriko yaliyotokea katika Ukanda wa SADC kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2022.

Post a Comment

0 Comments