DCEA yashirikiana na vyombo vya ulinzi kuteketeza hekari 21 za mashamba ya bangi mkoani Arusha

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kuanzia Mei 20 hadi 23,2022 Mei 2022 mkoani Arusha, ilifanya operesheni katika maeneo mbalimbali mkoani humo na kufanikisha kuteketeza zaidi ya hekari 21 za mashamba ya dawa za kulevya aina ya bangi.
Kamishna Jenerali wa mamalaka hiyo, Bw. Gerald Musabila Kusaya.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Mei 24, 2022 na Afisa Habari Mwandamizi Serikalini kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Daniel Kasokola kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa mamalaka hiyo, Bw. Gerald Musabila Kusaya.
Katika operesheni hiyo takribani kilo 220 za bangi zilikamatwa katika eneo la Usa river wilaya ya Arumeru na Wilaya ya Monduli jijini humo. 

Vilevile watu wanne wanashikiliwa kwa tuhuma za uzalishaji na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Mamlaka inatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kutoa taarifa juu ya watu wanaojihusisha na uzalishaji na usambazaji dawa za kulevya. Kata dawa za kulevya timiza malengo yako.

Post a Comment

0 Comments