TAKUKURU yatoa onyo kwa watendaji wanaoshirikiana na matapeli wa ardhi Pwani

NA DIRAMAKINI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imetoa tahadhari kwa watendaji wa serikali wanaoshirikiana na matapeli wa ardhi na kusisitiza kuwa dawa yao wanayo.
Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani, Christopher Myava alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Myava amesema kuwa, baadhi ya matapeli wa ardhi wamekuwa wakitumia vitendo vya rushwa na kusababisha migogoro isiyokwisha ambayo iko mahakamani.

Amesema kuwa, baadhi ya watendaji wa serikali wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kushirikiana na matapeli wajue wanawafuatilia ili kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Kwa upande wa rushwa kwenye chaguzi za ndani za vyama amesema, watazifuatilia ili kukabiliana na viongozi wanaotoa rushwa kupata uongozi kwani ni kinyume cha sheria.

Ameongeza kuwa, kwenye chaguzi hizo na hawatakaa nyuma bali watajikita katika kutoa elimu juu ya madhara ya rushwa ili wananchi waweze kuchagua viongozi safi wasiyotokana na rushwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news