Emmanuel Kihaule:Haijalishi kipato chako, usipojipanga vyema utabaki hoi kifedha kila siku!

NA DIRAMAKINI

ANAANDIKA Emmanuel Kihaule....

Niliwahi kufanya kazi na taasisi moja ya kimataifa miaka kama kumi iliyopita ambapo nilikuta watu waliofanya kazi kwa muda sawa sawa na umri wangu wakati huo. 

Maana yake wakati nazaliwa wao walikuwa kazini tayari! Lakini ilipotokea msahahara ukachelewa tu, wapo walioacha magari kwenye parking na kurudi nyumbani kwa lifti au daladala kwa kukosa mafuta!
Kwenye taasisi nyingine nyingi dada au kaka wa chai pamoja na madereva ambao wana vipato vya chini ndio huwakopesha hela, huduma (zikiwemo vocha, luku n.k.) na bidhaa mabosi wao wanolipwa karibu mishahara yao ya mwaka mzima kwa mwezi mmoja tu!

Hawa jamaa hawaoni aibu kukaa kwenye maeneo yanayochukuliwa kuwa ni wenye elimu ndogo, kuhamia kwenye nyumba yenye matoleo nje (ambayo haijaisha), kutumia magari yao kama taxi weekend au siku za mapumziko. Hawa 'mabosi' siku hizi ni za kula na kunywa na marafiki na kwenda kutembea sehemu zenye gharama kubwa. Ni mabingwa pia wa kutengeneza visherehe visivyo na kichwa wala miguu. 

Party after party! Hawa maskini hujitajihidi kusomesha watoto wao shule za kawaida lakini zenye elimu bora pia (hawashindani na wengine bali huangalia uwezo na kipato chao), wanaendesha magari yenye kubana matumizi ya mafuta au hawaoni aibu kupanda daladala au bodaboda/bajaj, wanafanya biashara ndogondogo za kuleta mayai, vitafunwa, mbogamboga, vocha, mashine ya luku na kadhalika maofisini bila aibu.

Uchakarikaji huu pia huwaridhisha watoto wao wakati wale wa boss ni TV na katuni muda wote. Ikitokea bahati mbaya wazazi wa hawa watoto wa boss wakafariki au kutikisika kwenye kipato, watoto hawa huteseka sana kuhimili mabadiliko. Wengine huachwa kwenye nyumba za kupanga, wengine hulazimishwa kwenda kuishi vijijini kwa babu na bibi kwenye maisha magumu, wengine uhamishwa shule na wengine hukatisha masomo kabisa! Nawajua kadhaa ambao baada ya kupoteza hawakuwahi kurudi kwenye mstari tena!

Huyu 'maskini' hapo hapo nyumbani ana wapangaji karibia kumi wa chumba kimoja kimoja au viwili wanaomuita baba au mama mwenye nyumba wakati mabosi wake wanashindana kupanga nyumba bora maeneo yenye hadhi huku wakiwa na mikopo kazini, benki na hata kwenye taasisi nyingine za fedha kutokana na kuishi maisha yasiyo halisi! Waingereza wanaita High Flying Life au Riding a High Horse!. 

Unakuta hata gari lililonunuliwa kwa mkopo wa mshahara benki, kadi yake ipo kwenye taasisi nyingine ya fedha (mara nyingi ni zile za wapigaji au kwa kimombo money sharks). 

Wapo wengi ambao hushindwa kulipa mikopo hii kutokana na riba kubwa na kuishia kunyang'anywa haya magari. Ukienda kwenye yards za hizi taasisi utakuta zimejaa magari walionyang'anywa hawa 'mabosi'!

Kujivuruga kwenye vumbi na kuwa na mipango thabiti ya kujitegemea kifedha ni muhimu! Hakuna siku utasema umepata fedha za kutosha. Hicho hicho unachokipata sasa kinaweza kutosha kufanya mengi.

Ni kujipanga tu!

#kuchakarika
Emmanuel Kihaule
Mei 25, 2022

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news