Hamasa ya Sensa ya Watu na Makazi yashika kasi nchini, Dkt.Jingu asema kila mmoja asaidie kufikisha taarifa hizo njema kwa Watanzania popote walipo

NA DIRAMAKINI

WAFANYABIASHARA nchini wameshauriwa kufanyia kazi wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wa kusaidia kuweka matangazo ya nembo ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye bidhaa mbalimbali ili kuhamasisha zoezi hilo nchi nzima.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Sensa ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Dkt. John Jingu (wa kwanza upande wa kushoto) akitazama ripoti ya taarifa ya Sensa ya Watu na Makazi iliyoandaliwa mahsusi kuelekea zoezi linatorajiwa kufanyika nchini kote, Agosti 23, 2022.

Dkt.John Jingu ameyasema hayo leo Mei 26,2022 jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wawakilishi wa Sekta Binafsi na Wafanyabiashara kuelekea katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23,mwaka huu.
Amesema, licha ya maandalizi hayo kufika asilimia 80, kazi ya kukamilisha na kufanikisha zoezi hilo kwa asilimia zote 100 inaendelea sehemu mbalimbali nchini bila kuchoka.
"Sensa hii itakuwa ni sensa ya sita tangu nchi yetu ilivyoanza, hivyo ni jambo kubwa ambalo linafanyika kila baada ya miaka 10 na mwaka huu tuna bahati ya fursa ya kufanya sensa ya kitaifa,"amesema Dkt. Jingu.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza kutoka Zanzibar, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Thabit Faina amesema suala la uhamasishaji wa sensa linakwenda vizuri kwa kiasi kikubwa na sasa wamebakisha hatua ndogo ya asilimia 20.
Faina amesema, matarajio yao ni kuona wapi panahitaji huduma ya afya, kujenga shule mpya, kuwekeza aina ya biashara mbalimbali katika maeneo tofautitofauti.

Akizungumza kwa niaba ya Sekta Binafsi, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Paul Makanza amesema kupitia zoezi hilo la sensa, sekta binafsi itafaidika na takwimu hizo za idadi ya watu na makazi na kuzifanyia kazi ipasavyo hususani katika Sekta ya Biashara kulingana na uhusiano wa sekta hiyo na idadi ya watu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news