Ihefu FC yarejea tena Ligi Kuu ya NBC, msimu uliopita jahazi lilizamishwa na KMC FC

NA DIRAMAKINI

IHEFU FC kutoka Mbalizi mkoani Mbeya imefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Pan Africans.
Timu hiyo inaungana na DTB ya Dar es Salaam kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambazo zimemaliza msimu kwa kuwania ubingwa wa Championship nchini.

Ihefu ilishuka daraja msimu uliopita baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na KMC kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu uliopigwa Julai 19,2021 kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Huo ulikuwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu Bara, ambapo Ihefu ilishuka tena na kurudi Ligi Daraja la Kwanza baada ya kumaliza ligi ikiwa na alama chache (35) ambapo iliungana na Mwadui na timu nyingine mbili kushuka daraja moja kwa moja.

Post a Comment

0 Comments