James Mbatia, Angelina Mtahiwa wasimamishwa kazi NCCR-Mageuzi

NA DIRAMAKINI

HALMASHAURI Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. James Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shughuli zozote za chama hadi mkutano mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma zinazowakabali.

Uamuzi huo umefikiwa leo Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu ndani ya chama hicho cha upinzani nchini.
Bw.Joseph Selasini ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa Azimio hilo amesema kuwa,licha ya kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazotolewa hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments