Kigogo wa AMCOS ajinyonga baada ya kuoneshwa rangi ya Rais Samia na RC Kafulila

NA DIRAMAKINI

DANIEL Jilala mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni Katibu wa Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) mkazi wa Kijiji cha Sulu Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu amekutwa amejinyonga kwa kamba katika mti jioni ya Mei 27, 2022.

Marehemu ameacha ujumbe wa simu (sms) aliomtumia mmoja wa afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ulioshiria kuwa, muhanga wa operesheni inayoendeshwa na RC Kafulila mkoani Simiyu kusafisha uozo ndani ya ushirika, operesheni yenye baraka za Rais Samia Suluhu Hassan.
Simu ya marehemu imekutwa na ujumbe aliomtumia mmoja wa maofisa TAKUKURU wilaya Maswa mwenye namba 0622591912 uliosomeka;

"NIMEAMUA KUJIUA KWA SABABU SIJASAIDIWA, NAOMBWA RUSHWA KILA SIKU NA AFISA USHIRIKA BUDODI KUWA ANAWAPELEKEA TAKUKURU MKOA, LAKINI SIONI MATUMAINI YA SUALA LANGU NA INAELEKEA NITAFUNGWA, SASA SIONI SABABU KUISHI KWANI SIJUI WANANGU WATAISHIJE IKIWA NITAFUNGWA"

Aprili 4, 2022 akigawa pikipiki Dodoma kwa maofisa ugani nchi nzima tukio lilioandaliwa na Wizara ya Kilimo, Rais Samia Suluhu Hassan alimwelekeza Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Kafulila kuendelea kudhibiti wizi wa pembejeo za pamba na michezo michafu kwenye vyama vya ushirika na ushirika..

"Nakuagiza Kafulila, endelea kuwakaba, najua wapo ambao mliowafungulia mpaka kesi za uhujumu uchumi kwa wizi wa madawa ya pamba. Nasisitiza endelea kuwakaba wezi wa pembejeo na ushirika wote tena kwa hatua kali mpaka wazijue rangi zangu,"aliagiza Rais Samia.

Katika utekelezaji huo, RC Kafulila aliwaondoa maofisa ushirika wote ngazi ya wilaya na kuelekeza wapangiwe kazi zingine wilayani kwani ni sehemu ya madhaifu ya usimamizi wa ushirika na hujuma kwa wakulima wa pamba.

Mpaka sasa vyama vya msingi 182 kati ya 335 vimefanyiwa uchunguzi na TAKUKURU ambapo nyingi zimerejesha fedha ama za wakulima au wanunuzi na kubaki AMCOS 37.

Post a Comment

0 Comments