Kwa nini iwe Profesa Edward Hoseah tena?

NA DIRAMAKINI

NI kwa sababu, Profesa Edward Hoseah ndani ya mwaka mmoja anaomaliza akiwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kupitia uongozi wake wamefanikiwa kutekeleza kikamilifu ahadi alizotoa awali.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ndani ya uongozi wake wa mwaka mmoja akiwa TLS ni kushughulikia malalamiko dhidi ya mawakili wao kwa kutumia taratibu za ndani ya chama. Hadi sasa ndani ya chama hicho hakuna wakili aliyeadhibiwa au kuvuliwa uwakili wake.

Aidha, kupitia uongozi wake wa mwaka mmoja wamefanikiwa kuishawishi Serikali kufanya maboresho ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Kutokana na majadiliano yenye tija baina ya TLS na Serikali, hivi sasa mashaurin yote ya jinai yatapelekwa mahakamani baada ya ushahidi kukamilika. Maboresho hayo yanalenga kupunguza msongamano wa mahabusu gerezani na kuwasaidia wananchi.

Profesa Hoseah anamaliza muda wake huku akiomba ridhaa tena ya kutetea nafasi hiyo kupitia uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya mwezi huu. Tazama mambo mengine mazuri yaliyofanywa na uongozi wake hapa chini;

Mgombea Urais wa TLS 2021, Albert Msando anena?

Shemzad Amir Walli naye afunguka

SAFARI YA KITAALUMA

Profesa Hoseah mwaka 1985 alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, akishinda pia Tuzo ya Mwanafunzi Bora ya Kitivo cha Sheria katika "Constitution Law".
 
- Mwaka 1989 alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Sheria (LLM) ya Chuo Kikuu cha Queens, Ontario, nchini Canada na kupewa Tuzo ya Mwanafunzi Bora ya Chuo Kikuu cha Queens.

- Mwaka 2007 alitunukiwa Shahada ya Uzamifu (PhD) katika Sheria ya Chuo kikuu cha Dar es salaam akibobea katika "Law of Evidence".

- Mafunzo katika Sera, Uongozi, Maadili na Kukabiliana na Rushwa katika Vyuo na Taasisi zifuatazo; Chuo Kikuu cha Passau (2007), Chuo kikuu cha Birmingham (2003) na Taasisi ya Benki ya Dunia (WI) mwaka 1998.

- Mwaka 1997 alihitimu Astashahada ya Utatuzi wa Migogoro kutoka katika Kituo cha Diplomasia (CFR) nchini Tanzania.

UZOEFU NA UBOBEZI KATIKA SHERIA

- Mhadhiri katika kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ( Law of Evidence and Legal Practice)

- Mhadhiri katika Kituo cha Diplomasia (CFR) akifundisha Sheria katika Biashara za kimataifa na uwekezaji.

- Mwanazuoni (Visiting Scholar) katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern, Chicago (2003-2005)

- Profesa wa muda (Adjunct Professor) wa Shule ya Sheria ya Duke Nchini Marekani (2010 - 2012).

- Tuzo kutoka katika Taasisi ya kimataifa kwa mchango katika maboresho ya Sheria ya Jinai (2003).

- Wakili na Mkurugenzi katika Hosea & Co Advocates wabobezi na watoa huduma mbalimbali za kisheria.

- Mkufunzi wa Taasisi ya "Uongozi Institute" kuanzia mwaka 2019

- Profesa katika Chuo Kikuu cha Iringa kuanzia mwaka 2021

- Mwandishi wa vitabu na machapisho ya kitaaluma.

- Mjumbe wa Bodi mbalimbali na mshauri wa masuala ya kitaalam katika mawanda ya Sheria.

UZOEFU KATIKA SHUGHULI ZA UONGOZI

- Rais wa sasa wa Tanganyika Law Society (TLS) kuanzia mwaka 2021.

- Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania.

- Rais wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa Afrika Mashariki (2008-2010, 2014-2015).

- Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC ( SAFAC) mwaka 2010-2011.

- Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Afrika (AU) katika Mapambano ya Rushwa (2011-2012)

- Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukabiliana na Rushwa (IAACA, 2012-2015).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news