Mei Mosi yafana kwa wafanyakazi wa OR-TAMISEMI

NA ASILA TWAHA, OR-TAMISEMI

WAFANYAKAZI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) wameadhimisha Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi 2022 kwa kushiriki maandamano yaliyoanzia katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Central hadi Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Akiwa ni mgeni rasmi wa Sikukuu ya Mei Mosi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema, anatambua mchango mkubwa walionao wafanyakazi katika kuchangia uchumi wa nchi na kusema, wafanyakazi hao waendelee kufanya kazi kwa kujituma na uadililifu akiahidi Serikali itaendelea kufanyia kazi maombi yaliyowasilishwa na Chama cha Wafanyakazi.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kaika maadhimisho ambayo Kitaifa yamefanyika jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Henry Makunda amesema, sababu ya kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ndio kilio chetu Kazi Iendelee”.
"Inamaanisha ni muda wa miaka kadhaa tangu wafanyakazi kuongezwa mshahara ikiwa kwa sekta binfasi takribani miaka tisa na seka za umma ni miaka saba,"amesema huku akifafanua kuwa, hali hiyo inapelekea kupungua kwa ari ya utendaji kazi kwa wafanyakazi hao.

Aidha, amesema kwa sasa kima cha chini kwa sekta binafsi ni shilingi 400,000 na kwa upande wa umma kima cha chini ni shilingi 300,000 ambapo kima hicho kilitangazwa mwaka 2015.
“Pamoja na nchi yetu kukumbwa na ugonjwa wa UVIKO-19 na kwa nchi za wenzetu Ukraine na Urusi kuwa na vita ambapo imesababisha kushuka kwa uchumi tunaomba Serikali iangalie namna ya kuongeza mishahara kwa wafanyakazi ili kuwezesha kuendelea kumudu gharama za maisha,”amesema Makunda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news