Mzazi mkanye mwanao:'Panya Road' 31 mikononi mwa Jeshi la Polisi Dar es Salaam, msako waendelea mtaa kwa mtaa

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata vijana 31 wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu maarufu Panya Road kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uporaji baada ya kuvunja nyumba, kujeruhi na kuiba vitu mbalimbali vya nyumbani.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa jana Mei 6, 22 ikiwa ni matokeo ya operesheni maalum na msako wa mtaa kwa mtaa dhidi ya vijana wanaojihusisha na Makundi ya Panya Road.

Kamanda Muliro amesema kuwa, operesheni hiyo ambayo ni endelevu ilianza April 27, 2022 na imefanikiwa kuwakamata Wahalifu hao ambao wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 13-20 na wakati wanafanya uhalifu wanatumia mapanga, visu, nondo, na mikasi mikubwa.

Amesema, watuhumiwa hao walifanyiwa mahojiano ya kina ambapo walibainika kuhusika katika vitendo vya kihalifu na kuonesha baadhi ya vitu walivyoiba zikiwemo TV 12 na simu 4 za mkononi.

Aidha,Kamanda Murilo ametoa onyo kali na kueleza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuwakamata ambao wamekuwa wakipokea mali mbalimbali za wizi zinazotokana na matukio ya kihalifu.

"Jeshi la Polisi halitasita kuwafikisha kwenye vyombo vingine vya kisheria wanaoshirikiana na wahalifu," amesema Kamanda Muliro

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Serikali kupitia Jeshi la polisi linatakiwa kudhibiti matukio ya kihalifu kwa kukabiliana na wahalifu hao, kwanza wwahakikishe vijiwe vyote vya wahuni vinasambaratishwa, wazazi kutoa taarifa iwapo watabaini mienendo isiyofaa kwa watoto wao, wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka ili kuchukua hatua stahiki. Pia, wajumbe wa nyumba kumi na wenyeviti wa serikali za mitaa wawajue watu wanaowaongoza na kuwatambua wageni wanaofika kuishi aisha kwa ndugu na jamaa zao au wapangaji. Tushirikiane kuimarisha usalama kwa jamii

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news