Naibu Waziri Chillo asisitiza umuhimu wa elimu matumizi ya ardhi

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Khamis Hamza Chillo amewataka viongozi wa mkoa na wilaya nchini kuhakikisha wanawaelimisha wananchi namna bora ya matumizi ya ardhi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Khamis Hamza Chillo akizungumza wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili, 2022 mkoani humo.

Chillo alitoa kauli hiyo Aprili 30, 2022 wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kupeleka mrejesho wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

“Twendeni tukawaambie watu namna bora ya utumiaji au matumizi bora ya ardhi, ardhi hizi tunaziumiza kuna shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika ardhi mwisho wa siku tunaiharibu ardhi,”alisema Chillo.Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili 2022 mkoani humo. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza kwenye mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili, 2022 mkoani humo. 

Aliwataka viongozi hao wa mkoa na wilaya kwenda kuwafahamisha wananchi namna ya kufanya shughuli za kibinadamu bila kuchafua mazingira au kuharibu ardhi.

“Kuna shughuli nyingi za kibinadamu zinafanyika kama vile ujenzi wa makazi usiozingatia taratibu na mwisho wa siku ardhi inaharibika na pale inapoharibika basi na mazingira nayo hayatakuwa salama,” alisema Naibu Waziri Chillo.
Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili 2022 mkoani humo. Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Meryprica Mahundi akizungumza katika mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili, 2022 mkoani humo.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta, Dkt.Angeline Mabula alieleza kuwa, ni jukumu la viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji kuhakikisha wanalinda maeneo yote ya hifadhi kwa lengo la kuepuka uharibifu unaoweza kutokea.

Akigeukia utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini, Dkt Mabula alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa na migogoro kwenye vijiji 12 ambapo kati ya vijiji hivyo vijiji 8 Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuendelea kubaki kwenye maeneo yake huku vijiji 4 vikitakuwa kufanyiwa tathmini.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja akizungumza kwenye mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili 2022 mkoani humo. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili, 2022 mkoani humo. Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza kwenye mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 30 Aprili, 2022 mkoani humo. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

“Kati ya vijiji 12 vilivyoingia kwenye migogoro ya matumizi ya ardhi na maeneo ya hifadhi hapa Kilimanjaro vijiji 8 mhe rais ameridhia vibaki. Si jambo jepesi watu kuvunja sheria na kutakiwa kubaki, nisisitize watu wasiendelee kuvunja sheria na kusubiri huruma ya rais,” alisema Dkt.Mabula.

Timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta bado inaendelea na ziara zake katika mikoa mbalimbali nchini kupeleka mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye vijiji 975 ambapo katika awamu hii ya pili timu ya Mawaziri hao imetembelea mikoa ya Pwani, Tanga, Morogoro, Mara na Arusha.

Post a Comment

0 Comments