NBS NA OCGS:Hatujatangaza nafasi za kazi za Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, kuweni makini

NA DIRAMAKINI

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) zimewataka wananchi wote kuchukua tahadhari kutokana na taarifa zinazoendelea kusambaa kwa kasi mitandaoni zikielezea kuwa wametangaza nafasi za kazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma,inaeleza kuwa,hadi sasa ofisi hizo hazijatangaza nafasi za kazi za Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Post a Comment

0 Comments