TANAPA:Hakuna raia waliopotea Serengeti

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa kisemacho, 'Serengeti: Wanaodhaniwa Askari wa Wanyamapori Watuhumiwa kwa Utekaji'.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Mei 2, 2022 na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Habari na Mawasiliano-TANAPA, Bw.Pascal Shelutete imefafanua kuwa, shirika halijapokea taarifa zozote rasmi juu ya askari wake kuwapiga na kuwateka wananchi.

Sambamba na baadhi ya watu kupotea katika mazingira tata ya eneo la hifadhi. "Tunaendelea kusisitia kwa wanaoendesha mitandao ya kijamii kuwa makini na taarifa wanazozisambaza ili kutoleata taharuki kwa jamii hususani katika masuala yahusuyo maisha ya binadamu,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo;

Post a Comment

0 Comments