Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi watatu

NA  GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi watatu.

Mosi amemteua Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar akichukua nafasi ya Sheikh Khamis Haji Kamis ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo, Sheikh Hassan alikuwa Naibu Kadhi Mkuu na Kaimu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 5, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said uteuzi huo umeanza tarehe tajwa.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Sheikh Othman Ame Chum kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, Sheikh Othman alikuwa Mrajis wa Mahakama ya Kadhi.

Uteuzi wa tatu, kwa mujibu wa taarifa hiyo ni wa Bw. Rashid Khamis Othman ambaye Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua kuwa Kamishna wa Kazi Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo Bw.Rashid alikuwa Afisa Kazi Mwandamizi Mkoa wa Kaskazini na Kaimu Kamishna wa Kazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Post a Comment

0 Comments