Rais Samia ampa maagizo Waziri Bashungwa kuhusu fedha za UVIKO-19

NA ANGELA MSIBIRA,OR-TAMISEMI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa kusimamia tenda za ununuzi wa vifaa tiba na kazi zingine kupitia fedha za UVIKO-19.
Akiongea na wananchi wa Uyui mkoani Tabora leo Mei 17, 2022 kwenye ufunguzi wa barabara ya Nyahua –Chanya- Uyui-Tabora, Rais Samia amesema kuna zabuni za ununuzi wa vifaa vya afya bado zinasuasua kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mhe.Rais Samia anafafanua kuwa, mwisho wa matumizi ya fedha za UVIKO-19 ni mwezi Juni, 2022 hivyo fedha zote zinahitajika kutumiwa kwa wakati ili kukidhi vigezo vya kuoa fedha zaidi, amemuagiza Waziri Bashungwa kuhakikisha zabuni hizo zinafanyiwa kazi kwa wakati ili kazi hizo zikamilike kwa wakati.
“Ucheleweshaji wa zabuni hizo utasababisha fedha nyingi kutotumika kwa wakati na kusababisha ukiukwaji wa malengo ya fedha hizo, suala hilo litapelekea fedha kurudishwa na kukosa fedha nyingine za maendeleo, nakuagiza Waziri wa TAMISEMI kalisimamie hili,”amesema Rais Samia.

Kuhusu matumizi ya fedha kwenye Halmashauri Rais Samia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia fedha zinazotolewa na Serikali kwa kazi zilizokusudiwa za kutatua kero za wananchi
Amesema, Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwenye ngazi ya Halmashauri lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi katika Sekta ya Afya, Elimu, Maji hivyo zisimamie na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

Aidha, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo, meza, ujenzi wa maabara, ununuzi wa viti na ujenzi wa nyumba za waalimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news