Prof.Shemdoe:Wakurugenzi 59 warejeshe fedha za bakaa, kujibu hoja za CAG

NA ANGELA MSIMBIRA, OR-TAMISEMI

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri 59 kuhakikisha wanarejesha fedha za bakaa na kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Ametoa agizo hilo leo 17 Mei, 2022 kwenye kikao kazi na Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo walifunga mwaka na bakaa hasi katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Prof. Shemdoe amefafanua kuwa, katika ukaguzi uliofanywa na CAG katika mwaka wa fedha 2020/21 hoja kubwa ni halmashauri hizo kutumia fedha kwenye kazi sahihi lakini na kuahindwa kuziripotia ipasavyo.
Ametaja sababu zilizopelekea kutokea kwa dosari hizo ni halmashauri kuhamisha fedha za ujenzi wa majengo ya utawala na hospitali za wilaya katika akaunti ya amana ambazo zilisalia mwishoni mwa mwaka kabla ya kupata kibali cha uhamisho kwa kuwa kibali kilitoka kilitoka kwa kuchelewa.

Aidha, halmashauri zilifanya malipo ya Dummy Exchequer kwenda kwenye vituo vya afya na zahanati ikiwa mgawanyo ulishapelekwa na hazina pamoja na malipo kuvuka mwaka mwingine wa fedha,
Amesema, halmashauri 37 zinatakiwa kurejesha kiasi cha shilingi bilioni 2.565 katika akaunti jumuishi (Treasury Single Account) na halmashauri 22 zinatakiwa kurejesha kiasi cha shilingi bilioni 1.177 kwenye akaunti za pamoja za Halmashauri ili kujibu hoja za CAG

Amezitaka halmashauri hizo kuhakikisha zinarejesha fedha hizo kwa wakati na kufanya usuluhishi wa kifedha kwa kutoa nyaraka zinazotakiwa ili hoja hizo zimalizike kwa wakati na kama fedha zilitumika na kutakiwa kurejeshwa za mapato ya ndani ni kiasi gani kilitakiwa kurejeshwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news