Rais Samia ateta na viongozi wakuu wa CHADEMA katika Ikulu ya Chamwino


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022. Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo katika Kikao cha pamoja na Wajumbe wa CHADEMA, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana mara baada ya Kikao kilichofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na Baadhi ya Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Baadhi ya Viongozi wa CCM pamoja na Serikali Ikulu Chamwino tarehe 20 Mei, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news