RC Mhandisi Gabriel awafunda vijana Mwanza

NA SHEILA KATIKULA

VIJANA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mwanza wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kulijenga taifa lao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel kwenye kikao cha Baraza la Kuu la umoja huo kilichofanyika jijini hapa wakati akizungumza na vijana hao.

Amesema, ni vema vijana kuchangamkia fursa zilizopo kwa kufanya kazi kwa weledi na kujiepusha na makundi hatarishi ambayo hayajitambui.

"Fichua kila aina ya vitendo vya uovu kwa kupaza sauti ili kuweza kukomesha uhalifu.Usiruhusu mtu yoyote akudharau, jiamini kwani kesho yako ni nzuri kuliko leo usirudi nyuma fanya kazi kwa bidii. Njia za siasa zina mafanikio, lakini hauwezi kufika huko mpaka upite kwenye umoja huu,"amesema Mhandisi Gabriel.
Naye Katibu wa UVCCM Mkoa Mwanza, Dennis Kankono amesema, wameamua kutumia baraza hilo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ssamia Suluhu Hassan kwa kupewa tuzo ya Babacar Ndiaye ya mwaka 2022 inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Jonas Rufungulo amesema, baraza hilo linalojumuisha viongozi wa umoja huo limekutana kwa lengo la kumuunga mkono Rais kwa kazi za kimaendeleo.

Kwa upande wake Mhamasishaji wa waendesha bodaboda nchi nzima, Abdalah Kibajaji amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwawezesha kwenye vyama vyao ili waweze kutambulika kama wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga alivyoboreshewa ofisi zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

2 Comments

Previous Post Next Post

International news