Simba SC yazidi kuikimbiza Yanga SC, yaichapa Ruvu Shooting 4-1

NA DIRAMAKINI

SIMBA SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Ni kupitia mtanange uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Mei 8,2022.

Kibu Dennis dakika ya 39, Rally Bwalya dakika ya 66, Nahodha John Bocco dakika ya 81 na beki Inonga Baka (Varane) dakika ya 85 ndiyo walioiwezesha Simba SC kujinyakulia alama tatu zikisindikizwa na mabao manne.

Kwa upande wa bao la Ruvu Shooting limefungwa na Haroun Athumani Chanongo akiiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 83.

Ni kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha alama 46, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa alama 10 na watani, Yanga baada ya wote kucheza mechi 22 kuelekea mechi nane za kukamilisha msimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news