TMEPiD YAENDESHA MAFUNZO YA UHAMASISHAJI USHIRIKI SAWA WA WANAUME KATIKA AFYA YA UZAZI NA MAENDELEO

NA KADAMA MALUNDE

SHIRIKA la Tanzania Men as Equal Partner in Development (TMEPiD) linalojihusisha na masuala ya uhamasishaji Ushiriki sawa wa wanaume wa Tanzania katika Afya ya uzazi na maendeleo limeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo Wawezeshaji ngazi ya jamii kutoa elimu ya Afya ya uzazi, ukatili kwa wanawake na watoto, umuhimu kutumia huduma za Afya uzazi kwa kuwalenga wanaume katika jamii wilaya ya Kahama na Kishapu mkoani Shinyanga.
Mratibu wa Mradi wa Ushiriki Sawa wa Wanaume katika Afya ya Uzazi na Maendeleo kutoka Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama mkoani Shinyanga. (Picha na Malunde 1 blog).

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Tanzania Men as Equal Partner in Development (TMEPiD) kwa ufadhili wa UNFPA yameanza kufanyika Mei 5,2022 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha washiriki wa mafunzo 15 kutoka wilaya ya Kahama na Kishapu ambako TMEPiD inatekeleza Mradi wa Ushiriki Sawa wa Wanaume katika Afya ya Uzazi na Maendeleo.
Mratibu wa Mradi wa Ushiriki Sawa wa Wanaume katika Afya ya Uzazi na Maendeleo kutoka Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kwenda kuelimisha makundi ya wanaume kuhusu afya ya uzazi na maendeleo
Mratibu wa Mradi wa Ushiriki Sawa wa Wanaume katika Afya ya Uzazi na Maendeleo kutoka Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kwenda kuelimisha makundi ya wanaume kuhusu afya ya uzazi na maendeleo.

Mratibu wa Mradi wa Ushiriki Sawa wa Wanaume katika Afya ya Uzazi na Maendeleo kutoka Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba amesema mara baada ya mafunzo hayo, TMEPiD inategema kutakuwepo na mabadiliko chanya katika kutumia huduma za Afya ya uzazi, kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuimarika kwa Afya katika jamii.

“TMEPiD inatekeleza mradi huu katika mikoa ya Dodoma, Mara, Dar es salaam, Unguja, Pemba na Shinyanga katika wilaya ya Kahama na Kishapu kwa ufadhili wa UNFPA. Kupitia mafunzo haya waelimishaji rika hawa watapewa mbinu shirikishi kwa ajili ya kuwafikia wanaume wengi zaidi.

“Tunaamini kabisa Wawezeshaji hawa/waelimisha rika hawa kutoka makundi mbalimbali yakiwemo ya waendesha bodaboda, madhehebu ya dini, wajasiriamali, wafugaji, jeshi la jadi sungusungu na dawati la jinsia watakuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii kuhusu masuala ya afya ya uzazi na mambo mengine kadha wa kadha ikiwemo madhara ya mimba na ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia, VVU na UKIMWI,”ameeleza Komba.
Mratibu wa Mradi wa Ushiriki Sawa wa Wanaume katika Afya ya Uzazi na Maendeleo kutoka Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kwenda kuelimisha makundi ya wanaume kuhusu afya ya uzazi na maendeleo.
Sehemu ya Wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini.
Sehemu ya Wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini.
Sehemu ya Wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama Mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini.
Sehemu ya Wawezeshaji wa elimu ya uzazi kwenye jamii kutoka wilaya ya Kishapu na Kahama Mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini.

Amesema, ili kuondokana na matukio ya ukatili wa kijinsia, mifumo dume katika familia na jamii ambapo maamuzi mengi yanatolewa na wanaume wanaendesha mafunzo hayo kwa kushirikisha wanaume (wawezeshaji) ambao watakwenda kuelimisha wanaume wenzao ili kuleta maendeleo na kuboresha afya ya jamii ikiwemo wanaume kushiriki katika kupanga uzazi wa mpango na kutunza familia.

“Zamani mambo ya uzazi yalichukuliwa kama ni ya wanawake tu, hili ni jambo la wote, sasa tunataka huduma shirikishi ya uzazi wa mpango (mwanaume na mwenzi wake), wanaume wengi wafikiwe na washiriki katika uhamasishaji wa afya ya uzazi, wanaume washiriki katika kupanga uzazi,kwenda hospitalini na wake zao,kujua makuzi ya mtoto, wawe na elimu ya kutosha kuhusu VVU na UKIMWI, wawe tayari kupiga vita mimba na ndoa za utotoni, wapinge ukatili wa kijinsia na kuhakikisha kuna maendeleo kwenye jamii,”amesema Komba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news