Uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) watoa ufafanuzi kuhusu ajali ya moto chuoni

NA DIRAMAKINI
"Tunautaarifu Umma wa watanzania kuwa leo tarehe 20 Mei 2022 majira kati ya saa 6
na saa 7 mchana ulitokea moto katika jengo moja lenye ofisi na mabweni ya wanafunzi.

Baada ya taarifa za moto kutolewa kwa uongozi wa Chuo, Jeshi la Zima moto na vyombo vya ulinzi na Usalama vilijulishwa na kuwasili mara moja ili kuhakikisha usalama wa mali na raia.

Jitihada za kuuzima moto zilifanywa na moto ulidhibitiwa baada ya muda mfupi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kikosi cha Zimamoto cha Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Tathimini ya awali inaonyesha kuwa madhara ya moto ni madogo. Hakuna mtu aliyedhurika wala nyaraka muhimu za Chuo zilizoathirika kutokana na moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika.

Kwa sasa Uongozi wa Chuo unaunda kamati ya kuchunguza chanzo cha moto na kufahamu athari halisi za moto huo.

Uongozi wa Chuo unashukuru vyombo vya ulinzi na usalama hususani Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, na Kikosi cha Zimamoto cha Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kudhibiti moto na hivyo kupunguza athari ambazo zingeweza kutokea"

Post a Comment

0 Comments