VIDEO:Tumeanza kupitia taarifa za watumishi, ifikapo Julai 2022 kila mtumishi atakuwa amepata mshahara mpya

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama amesema, utekelezaji wa maelekezo ya kuwapandisha mishahara Watumishi wa Umma, Mhe. Jenista amesema ofisi yake itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ifikapo Julai, 2022 kila mtumishi wa umma anapata mshahara mpya. Hivyo amewataka watumishi wa umma kuwa watulivu wakati zoezi hili likiendelea kushughulikiwa na Serikali.
“Mimi na watendaji wangu tumeanza kupitia taarifa za Watumishi katika Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara ili kushirikiana na Wizara ya Fedha katika kukamilisha zoezi la kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma, itakapofika Julai 2022 kila mtumishi atakuwa amepata mshahara mpya kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa ahadi ambazo Mhe. Rais amekuwa akizitoa kwa watumishi wa umma zimekuwa zikitekelezwa kwa wakati, hivyo jambo hili la mishahara litatekelezwa kama alivyokusudia.

Post a Comment

0 Comments