Waiheshimisha OR-TAMISEMI kupitia michezo ya Mei Mosi,Prof. Shemdoe awapa kongole

NA ASILA TWAHA, OR-TAMISEMI

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (0R-TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe amewapongeza wanamichezo wa TAMISEMI Sports Club kwa kushika nafasi za juu katika michezo ya Mei Mosi na kuwaambia nafasi hizo zinadhirisha kuwa, ushiriki wao katika michezo ulikuwa ni wakujituma katika kuipambania OR-TAMISEMI.
Prof. Shemdoe amesema hayo Aprili 30,2022 wakati akipokea kombe la timu hiyo ambapo Timu ya TAMISEMI Sports Club Riadha inaongoza kuwa washindi wa jumla wa michezo ya Mei Mosi kwa mwaka 2022 na kupata kombe la ushindi na medali.

Amesema, hata mchezo wa soka kushika nafasi ya pili inaonesha mapambano yalikuwa ni yenye kuonesha utafutaji wa kuwa mabingwa wa jumla wa mchezo huo.
“Nimefurahi sana TAMISEMI ni kubwa kwa kuonesha ushiriki wa kucheza mchezo wa riadha, kamba, football, kurusha tufe,baiskeli na kucheza karata inaonesha wazi kuwa ninyi ni wapambanaji niendelee kuwaomba endeleeni kujituma na sisi viongozi wenu tutaendelea kuwaunga mkono kwa kuwa pamoja nanyi kwa kuhakikisha mnaendeleza michezo ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, kanuni taratibu na nidhamu wakati wote wa michezo yenu,”amesema Prof. Shemdoe

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Victor Kategere awali amesema, pamoja na changamoto za kimchezo amemueleza Prof.Shemdoe timu ya TAMISEMI inauwezo mkubwa na endapo itaendelea kusimamiwa itafika mbali.
Amesema, mapambano walionesha tangu mwanzo wa michezo hivyo inastahili kuendelea kusapotiwa kwani michezo ni moja ya njia ya kujenga mahusiano mazuri, ajira lakini pia hujenga afya.
Naye Katibu wa TAMISEMI Sports Club, Alex Morice ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kuisimamia timu hiyo na kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake.

Pia ameomba uongozi huo uendelee kuisapoti kwani timu yao ya netiboli inategemea kwenda jijini Kampala nchini Uganda mwezi Mei, 2022 kwa ajili ya mshindano Klabu Bingwa Afrika Mashariki.
Timu ya TAMISEMI Sports Club riadha inakuwa mshindi wa jumla kwa Sikuku ya Wafanyakazi Mei Mosi mwaka 2022 ambapo inatarajiwa kupatiwa kombe la ushindi na mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news