WATANZANIA MUOMBEENI RAIS WENU WASEMA VIONGOZI WA DINI, KONGAMANO KUFANYIKA KESHO MBEYA

NA DIRAMAKINI

VIONGOZI wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wamewaasa Watanzania wote kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza vyema Taifa la Tanzania ili aweze kudumisha amani.
Wameyasema hayo leo Mei 30, 2022 kwenye mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika mkoani Mbeya ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye Kongamano la Kuliombea Taifa, Kumuombea Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kumpongeza kwa uongozi bora litakalofanyika kesho Mei 31, 2022 katika Ukumbi wa Tughimbe mkoani humo.

Kwa uapande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Katoliki Tanzania, Gervas Nyaisonga amesema kuwa, kila mmoja anapaswa kukubali na kutambua kwamba,jambo ambalo linalokusudiwa kesho ni nzuri na la heri.
"Ni jambo nzuri linalokusudia kuomba kwa ajili ya nchi yetu na kwa ajili ya viongozi wetu. Na vile vile kupongeza, ikiwa ni ishara ya kushukuru na kutambua jitihada zilizofanyika. Ninasema ni jambo nzuri kwa sababu namna ya kupata mahitaji ni kuomba, wengine wanapata mahitaji kwa kuomba, wengine wanapata mahitaji kwa kufanya kazi, wengine kwa kutafiti, hizo zote ni njia za kupata mahitaji.

"Sisi kama Watanzania tuna mahitaji, wenzetu wamesema hapa hitaji letu la kwanza na la msingi ni amani, na utulivu na mazingira mazuri ili shughuli zinazofanywa na watu kulingana na vipaji vyao ziendelee. Sasa hivi vitu vizuri huwa haviji hivi hivi, lazima kuvifanyia kazi,kuviomba kwa kuwa, tuna muamini Mungu, ninajua yote tuliyo nayo yanatoka kwa Mungu na sisi wenyewe ni wa kwake Mwenyenzi Mungu. Ndiyo maana ninasema ni jambo nzuri, kongamano la kesho tulipokee kwa moyo wa dhati na tujitoe kwa moyo, tujitoe kwa sababu hivi vitu vizuri haviji hivi hivi,"amesema.
Amesema kuwa, "tumekusanyika viongozi wa dini mbalimbali si mkoa tu, lakini tumekusanyika Kitaifa tuna viongozi mbalimbali wa Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi,kutoka mikoa mbalimbali Dar es Salaam mpaka Zanzibar tunao hapa. Na lengo kubwa tumeona kuna umuhimu kwa sababu sisi viongozi wa dini katika maandiko yote tumeamriwa tuwaombee viongozi, Wafalme na tukuiombea Wafalme tunatambua kabisa kuwa, kunahitajika amani ya nchi, utulivu, upendano ambalo;

Post a Comment

0 Comments