TBS yashiriki Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii jijini Tanga

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewahamasisha wananchi kutembelea banda lake katika Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii yanayoendelea katika Uwanja wa Mwahako jijini Tanga ili kupata huduma mbalimbali. Maonesho hayo ambayo yalianza Mei 28, 2022 yanatarajiwa kufikia tamati Juni 6, 2022.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ( Mb) akipokea zawadi kutoka kwa waandaaji wa maonesho iliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Adam Malima wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo mapema leo.

Maafisa wa TBS wakimuelekeza mzalishaji wa mafuta ya alizeti (Ashura Sunflower Oil) utaratibu wa kuthibitisha ubora wa bidhaa hiyo pindi alipotembelea banda la TBS katika maonesho ya biashara Tanga yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako.
Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi mapema leo na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji ( Mb).

Post a Comment

0 Comments