Waziri Bashungwa amshukuru Rais Samia kwa kuridhia nyongeza ya mishahara

NA ANGELA MSIMBIRA, OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 23.3.
Akitoa salamu za Ofisi ya Rais-TAMISEMI leo Mei 18, 2022 kwenye uzinduzi wa barabara Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa kilometa 342.9, uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Mhe.Bashungwa amesema asilimia 75 ya watumishi wanatoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo amemuahidi Rais kufanyakazi kwa weledi katika kuwatumikia wananchi.

Waziri Bashungwa pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge hadi kufikia asilimia 193 na kubadilisha mandhari ya eneo hilo.
Waziri Bashungwa anaendelea kufafanua kuwa kwa upande wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 1.1 na shilingi milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya.

Amesema, kwa upande wa ujenzi wa kituo cha afya Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Tutuo na kwa upande utatuzi wa changamoto za ujenzi wa nyumba za waalimu nchini katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 55.57 kwa ajili ya ujenzi huo
Waziri Bashungwa amesema, kwa upande wa ujenzi wa jengo la utawala Serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 700 na katika bajeti ya mwaka 2022/2023 zimetengwa shilingi milioni 600 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la utawala ili kusogeza huduma karibu na wananchi.  

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la anuani ya makazi na kujitokeza kuhesabiwa ili serikali iweze kuwatambua na kuweza kutoa huduma bora kulingana na takwimu zilizopo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news