Magazeti leo Machi 18,2026

Uzinduzi wa jukwaa jipya la kidijitali la biashara ya madini lijulikanalo kama Tellus Minerals B2B unatarajiwa kufungua fursa mpya za masoko ya kimataifa kwa wachimbaji wadogo na wa kati nchini Tanzania, kwa kuwaunganisha moja kwa moja na wanunuzi, wawekezaji na wadau wa sekta ya madini duniani.
Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Tellus Minerals B2B, Idrissa Songoro akizungumza jijini Dar es Salaam amesema, jukwaa hilo limeanzishwa kwa lengo la kuleta mabadiliko katika biashara ya madini duniani kwa kutoa mazingira ya wazi na huru ya kidijitali yanayowawezesha wadau kuthibitishwa na kuwasiliana moja kwa moja bila kupitia kwa madalali.

Alieleza kuwa, kupitia mfumo huo, wachimbaji na wazalishaji wa madini wanaweza kuunganishwa moja kwa moja na wanunuzi wa kimataifa pamoja na wawekezaji, jambo litakalowawezesha kufanya majadiliano ya kibiashara kwa uwazi na kujenga ushirikiano endelevu.Soma kwa kina hapa》》》

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here