Waziri Bashungwa atoa Siku 14 kodi ya pango Stendi ya Magufuli-Dar

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ametoa siku kumi na nne kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo, Kamati ya Fedha na uongozi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kufanya mapitio.

Sambamba na kupeleka mapendekezo ya changamoto za wapangaji katika kituo hicho ya kulalamikia kiwango kikubwa cha kodi ya pango ambapo wameeleza kwa sasa kiwango cha pango ni shilingi 40,000 kwa mita moja ya mraba.
Mheshimiwa Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Mei 30, 2022 wakati akikagua mradi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Magufuli Bus Terminal) kilichopo wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.

Pia ameagiza Mkurugenzi huyo kuondolewa kwa magari yote mabovu yaliyoegeshwa kwa muda mrefu ndani ya kituo hicho ambayo ni zaidi ya 40 yanayosababisha ufinyu wa eneo ili kutoa nafasi kwa magari mengine kupata maegesho ndani ya kituo.

Mwisho ameelekeza uongozi wa wilaya hiyo kuendelea kusimamia mpango uliopo kwenye ramani ya kituo hicho kwa kuweka kipaumbele cha kuboresha na kujenga miundombinu ya wafanyabiashara wadogo ili stendi hiyo iwe na manufaa kwa wanaanchi kulingana na Maelekezo ya Mheshimiwa Rais.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news