Waziri Bashungwa awaonya watumishi wa afya wenye lugha chafu kwa wagonjwa

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amewaagiza Waganga Wakuu Wa Mikoa kusimima nidhamu ya watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya msingi ikiwemo kutumia lugha mbaya na isiyo rafiki kwa wagojwa wakati wa utoaji huduma.
Bashungwa ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma katika kikao cha kujadili utekelezaji wa Mkataba wa afua za lishe nchini kilichowashirikisha Waganga wakuu wa Mikoa, Maafisa lishe wa Mkoa na wadau wa lishe Mei 26, 2022 amesema, alipokuwa mkoa Mara alikutana na kero za wananchi wakilalamikia baadhi ya wahudumu wa afya kutumia lugha chafu kwa wagonjwa.

“Kwenye ziara zangu nimekuwa nikikumbana na kero za wananchi wakati wakipatiwa huduma ikiwemo kauli zisizo rafiki kwa baadhi ya Wauguzi kwa wagojwa na nitumie nafasi hii kuwaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi katika vituo vyetu vya kutolea huduma,” amesema Bashungwa.

Bashugwa ameeleza kumekuwepo na changamoto ya kutopatikana kwa baadhi ya madawa ya kutosha ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wanaendelea kufuatilia na kuhakikisha fedha zilizopelekwa Wizara ya afya kupitia MSD yanapatikana madawa ya kutosha katika vituo vyote vya huduma za afya.
Aidha, amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa kuendelea kusimamia sehemu yao na kukwamua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayosuasua katika sekta ya afya ikiwemo ujenzi zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa Watanzania.
Vile vile, Bashungwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga fedha kiasi cha shilingi 1000 kwa kila mtoto aliye chini ya umri wa miaka mitano kwa ajili ya afua za lishe, pia kuhakikisha Mkataba wa lishe unatekelezwa kikamilifu na unakuwa dhana ya kutatua changamoto na kuleta tija kwa Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news