Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Mei 27,2022

NA GODFREY NNKO

LEO Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.59 na kuuzwa kwa shilingi 0.62 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.10 na kuuzwa kwa shilingi 50.54.
Aidha,Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.81 na kuuzwa kwa shilingi 1.83 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7488.4 na kuuzwa kwa shilingi 7552.9.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 27, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha, Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.60 na kuuzwa kwa shilingi 2.80 huku Metical ya Msumbiji (MZM) ikinunuliwa kwa shilingi 35.3 na kuuzwa kwa shilingi 35.6.
Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 340.2 na kuuzwa kwa shilingi 343.2 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 18.0 na kuuzwa kwa shilingi 18.2.

Post a Comment

0 Comments