Waziri Dkt.Kijaji: Mitambo ya KMTC iko salama na inafanya kazi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema mitambo iliyopo katika Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC) iko salama na inaendelea kufanya kazi ya uzalishaji wa vipuri na mashine mbalimbali wakati maboresho ya kuendesha mitambo hiyo kielektroniki yanaendelea.
Waziri Kijaji ameyasema hayo alipofanya ziara katika Kiwanda cha KMTC kichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro Mei 29, 2022 kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi na mikakati iliyopo ya kukifufua ili kifanye kazi kwa ufanisi na kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah pamoja na wajumne wengine aliziagiza Taasisi za TEMDO na CAMARTEC kufanya kazi kwa kushirikiana na kiwanda hicho ili kiweze kuzalisha bidhaa kwa wingi zilizosanifiwa na taasisi hizo.
Aidha, Waziri Kijaji alisema uboreshaji wa Kiwanda hicho ni muhimu kwa kuwa bidhaa za chuma zinahitajika katika matumizi mbalimbali ya kutengenezea mitambo, vipuru na bidhaa katika miradi ya kimkakati kama vile Reli ya Kisasa ya SGR na viwanda vingine vikubwa na vidogo.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolaus Herman Shombe amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha KMTC kinachozalisha bidhaa na vipuri mbalimbali vinavyotumika katika viwanda vingine. Kiwanda hicho kina ukubwa wa eneo la hekari 645 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vingine vitakavyokuwa vinatumia bidhaa za kiwanda hicho.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akitembelea Kiwanda cha Kilimanjaro Machine tools (KMTC) Mei 29, 2022 kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi na mikakati iliyopo ya kukifufua ili kifanye kazi kwa ufanisi na kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Akieleza umuhumu wa kufufua kiwanda hicho kwa Waziri Kijaji, Meneja Mkuu wa KMTC Bw. Adrian Nyabuki amesema mipango yote iliyowekwa ya kufufua kiwanda hicho ikitekelezwa itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vipuli na baadhi ya bidhaa za chuma nje ya nchi na kufanya vipuri na bidhaa hizo kupatikana kwa urahisi, kutoa ajira na kuchangia katika pato la taifa.

Wakati huo huo, Waziri kijaji akiwa ameambatana na ujumbe wake alitembelea Kiwanda cha kutengeneza magurudumu cha Arusha ( General Tyres ) kujionea mahitaji na mikakati iliyopo ya kufufua kiwanda hicho ili kiweze kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news