Waziri Dkt.Nchemba, wadau wa soka wajadili namna ya kuongeza ufanisi

NA SCOLA MALINGA-WFM

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na vilabu vya michezo pamoja na taasisi za Serikali zinazosimamia sekta hiyo ili kujadili mipango na mikakati ya kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza na viongozi wa vilabu vya michezo nchini kupitia Bodi ya Ligi, wakati alipokutana nao kuzungumzia maendeleo ya sekta ya mpira wa miguu pamoja na changamoto wanazopitia, kikao hicho kimefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam.(PiCHA NA WFM).

Wadau hao walimweleza Dkt. Nchemba kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika kuendeleza soka ikiwemo ufinyu wa bajeti katika Vilabu vyao pamoja na kuiomba Serikali iendelee kutoa nafuu zaidi ya kodi kwenye nyasi bandia pamoja na viunganishi vyake.

Dkt. Nchemba amewahakikishia wadau hao kwamba maelekezo ya Mheshimiwa Rais samia Suluhu Hassan aliyowapa ni kuhakikisha kuwa Sekta ya michezo inakuzwa kwa kuwa ni muhimu na vijana wengi wamejiajiri kupitia sekta hiyo.
Mchumi Mkuu aliyemwakilisha Kamishna wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Yosepha Tamamu, akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango na viongozi wa vilabu vya mpira wa miguu nchini, kupitia Bodi ya Ligi, mkutano huo ulifanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.

Alitoa wito kwa vyama vinavyosimamia michezo nchini kuhakikisha kuwa sekta hiyo inafanya vizuri ili kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania ndani na nje ya nchi pamoja na kuhakikisha kuwa miundombinu ya viwanja inajengwa kwenye maeneo ya kimkakati ili kukuza michezo nchini.

Aidha, Dkt. Nchemba amewaangiza wataalum wa Wizara ya Fedha na Mipango wapitie changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wadau pamoja na kuzipitia sharia za kodi ili kuendeleza sekta hiyo wakati huu ambapo bajeti ya Serikali inajadiliwa bungeni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na Makamu wa Pili wa Rais Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Bw. Steven Mnguto, akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba na viongozi wa vilabu vya michezo nchini, mkutano huo ulifanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya vilabu hivyo vya mpira wa miguu nchini, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Steven Mnguto, aliishukuru Serikali kwa kuthamini michezo na kuomba changamoto walizoziwasilisha kwake zifanyiwe kazi ili soka la Tanzania liweze kupiga hatua zaidi na kuzipa nafuu klabu ili ziweze kujiendesha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news