CCM Tabora yamweleza Rais Samia wanaridhishwa na utendaji wa Serikali yake

N DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Mei 18, 2022 ametembelea ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora, ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akiwasalimia baadhi ya viongozi wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tabora,mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za chama hicho leo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe,Balozi Batilda Buriani,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, Shaka Hamdu Shaka pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassan Mwakasubi.

Pamoja na mambo mengine, Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamati ya Siasa ya MKoa (CCM) kwenye Ofisi za chama hicho mkoani Tabora leo Mei 18, 2022 mara baada ya kutembelea ofisi hizo, ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.

Awali, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora, Hassan Mwakasubi akimkaribisha, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi mkoani Tabora na wananchi kwa ujumla wanaridhishwa na utendaji wa Serikali anayoiongoza katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
"Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora. Haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali, tunakushukuru sana na tunakukaribisha Tabora,"amesema Mwakasubi.

Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza Mei 17, 2022 na ataihitimisha Mei 19, 2022 kwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Mwenyekiti wao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao,mwisho kulia ni Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Taifa,Shaka Hamdu Shaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news