WAZIRI MBARAWA ARUHUSU MAGARI KUPITA JUU BARABARA YA CHANG'OMBE

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa leo ameruhusu kuanza kutumika kwa njia moja ya barabara ya Juu Chang'ombe ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kuanza kutumika kwa barabara hiyo, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS),Mhandisi Rogatus Mativila kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani kuhakikisha magari yanayotumia njia hiyo kwa sasa yanazingatia sheria za mwendo kwani bado ujenzi unaendelea eneo hilo.

Alisema kutumika kwa barabara hiyo kutasaidia kupunguza msongamano hivyo, kuwasaidia watumiaji wa barabara hiyo wapate muda wa kutosha kufanya shughuli zao kwani msongamano katika eneo hilo unawapotezea muda.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS,Mhandisi Mativila amemhakikishia Mhe. Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni Awamu ya Pili ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka BRT2 utakamilika kwa ubora na kwa wakati.
 
Mhandisi Mativila amesema ujenzi wote wa Barabara za Juu za Chang'ombe na Chuo cha Uhasibu unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments