Wizara ya Elimu kukutana na wabunge maboresho ya mitaala, sera

NA DIRAMAKINI

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatarajia kukutana na wabunge kwa lengo la kukusanya maoni kwa ajili ya kuboresha mitaala ya elimu na Sera ya Elimu ya Mwaka 2014.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mageuzi sekta ya elimu.

Mheshimiwa Waziri amesema, mkakati wa serikali ni kufanya maboresho ya sera na mitaa ya elimu, ambayo yatajikuta katika elimu ujuzi.

Amesema, Mei 7, mwaka huu watakutana na wabunge, ikiwa ni mwendelezo wa kupokea maoni ya kuboresha mitaala na sera ya elimu.

Amesema, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, yatafanyika mageuzi makubwa ya elimu, ambayo hayajawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru, ambapo rasimu ya mitaala mipya itatoka Desemba, mwaka huu.

"Kazi kubwa ya mitaala imefanyika na tumekusanya maoni zaidi ya 100,000, lakini ukikutana na mtu anakuuliza mnafanya nini kwenye elimu, sasa kutakuwa na makala kwenye televisheni,"amesema.

Pia amesema,wizara itaendesha kongamano kubwa la elimu mwishoni mwa mwezi huu na litafanyika kwa siku tatu, ambalo watapata maoni zaidi kuhusu maboresho hayo.

Post a Comment

0 Comments