NA MWANDISHI WETU
NUSU Fainali za Kombe la Shirikisho Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu Arusha na Mwanza.

Mwaka jana Simba waliifunga Yanga katika fainali 1-0 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, bao pekee la kiungo Mganda, Thadeo Lwanga.