Zuchu: Kuhusu Mtasubiri Sana, tumeonewa

NA DIRAMAKINI

MALKIA wa Wasafi Classic Baby (WCB), Zuchu amesema marufuku kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutoonyesha wimbo wa ‘Mtasubiri’ ulioimbwa na msanii Diamond Platnumz akimshirikisha yeye ni sawa na kuwaonea.
Zuchu ameyaeleza hayo Mei 7,2022 kupitia ukurasa wake wa kijamii akifafanua kuwa;

"Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia. Sijui nileleze vipi hisia zangu zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii bila ya kuchukuliwa kama mjeuri ila kwa hili mumetuonea .

Sisi ni vijana tunaotafuta rizki bila ya kuchoka lakini pengine Wazazi wetu, Basata Tanzania mmekua mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia muda vipaji na uwekezaji unaofanyika.

"Hapo awali mlitoa mirabaha Wasanii wa Wcb Hatukunusa Top List Wakati kitwakwimu za namba ,MAUZO na ufanyaji vizuri Katika Chati zote Kasoro yenu nyinyi Basata Tanzania Cosota Tanzania Nini shida wazazi wetu.Inawezekana vipi.

"Kisha hapo Tunalaumiwa kwa kutoshiriki Tuzo.Ni wazi kua Hii imekua wazi sasa kama mamlaka ya kisanaa inafanya kazi Kupinga juhudi za WCB lakini pengine hii hasira mnayoipandikiza juu yetu tunaihitaji kwa mafanikio chanya yetu na mashabiki zetu wanaotupigania.

"Mwisho niseme kazi iendelee Mashabiki zetu ,Maboss zetu mtusamahe sana kwa kero mnayokutana nayo haiko mikononi mwetu Wenye mamlaka washasema sisi ni nani? tuwe na subra na msituache mana nyinyi ndo kimbilio letu la mwisho Nawapenda sana.Sikukuu njema KAZI IENDELEE,''ameandika Zuchu.

Kilichojiri

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kuzifungia nyimbo ambazo inaona zimekosa maadili kwa jamii ambapo imepiga marufuku vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutoonyesha wimbo wa ‘Mtasubiri’ ulioimbwa na msanii Diamond Platnumz akimshirikisha Zuchu.

Wimbo huo umekuwa maarufu na unapendwa na watu wengi hasa vijana.

Kuzuiwa kwa video hiyo kumetangazwa kupitia taarifa ya TCRA na kuthibitishwa na Meneja wake wa huduma za utangazaji, Mhandisi Andrew Kisaka.

Katika tangazo hilo linaloonyesha limetolewa Aprili 29, 2022 ikiwa na kichwa cha habari ’Vyombo vya utangazaji kutopiga wimbo wa msanii Nasib Abdul (Diamond Platnumz) kwa kushirikiana na Zuhura Othuman Soud (Zuchu), uitwao ‘Mtasubiri Sana’.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa TCRA imepokea taarifa kutoka Basata ya kuzuia usambazaji wa video ya wimbo wa wasanii hao unaopigwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya utangazaji.

Imesema sababu za kuzuia video hiyo ni kutokana na kuwa na kipande kinaonyesha wahusika wapo kanisani wanaimba kwaya, lakini baadae wakaacha na kuelekea kwingine.

“Kipande hicho cha video kimeleta ukakasi miongoni mwa waumini wa madhehebu ya dini na kuleta hisia kwamba ni dharau juu ya dini au madhehebu fulani,"ilieleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news