Ajali ya basi la Zuberi yaua, kujeruhi mkoani Shinyanga

NA SAMIR SALUM (LANGO LA HABARI)

WATU watatu wamefariki dunia huku saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi lenye namba za usajili T435 DJS SCANIA kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi mkoani Shinyanga.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP George Kyando amesema kuwa, ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 15, 2022 majira ya saa nane mchana katika barabara ya Mwanza Shinyanga liligonga ukingo wa daraja na kutumbukia bondeni.

Kamanda Kyando ametaja mmoja wa waliofariki dunia kuwa ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Haule.

Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni dereva alipata tatizo la kiafya akiwa safarini.

Aidha, ametoa wito kwa madereva kuchunguza afya zao kabla ya kuanza safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news