Antonia Emmanuel apania kuweka historia mpya katika muziki wa injili Tanzania

NA DIRAMAKINI

MWIMBAJI wa muziki wa Injili kutoka mjini Morogoro, Antonia Emmanuel amewahakikishia watu wote watakaohudhuria uzinduzi wa albamu yake iitwayo Nasikia Maneno Maneno watabarikiwa sana.

Akizungumza na Famara Media, Antonia amesema kila kitu kinaenda vizuri katika maandalizi, na anachokifanya kwa sasa ni kuzidi kumalizia hatua zote ili afanye uzinduzi wa kihistoria mjini Morogoro katika kanisa la TGRC Mazimbu Barakuda.

"Maandalizi ya uzinduzi yanazidi kukamilika, kila idara husika inafanya kazi ili kuhakiki tamasha hili la Uzinduzi linafana sana na kuweka historia mpya katika tasnia ya muziki wa Injili Tanzania,"amesema Antonia Emmanuel.

Antonia amesema ana faraja maana watu mbalimbali walioalikwa wameonyesha mwitikio mkubwa wa kushiriki. Amewataja waimbaji na wageni waalikwa wamekuwa wakimpigia simu ili kujua maandalizi yanakwendaje, hii ikiwa ishara nzuri kuelekea kwenye kilele cha tamasha letu.
Bi. Emmanuel amesema amekuwa anapata sapoti kubwa kutoka kwa Mchungaji wake Jailos Maloda na wakristo wanaoabudu Kanisani hapo, hii ikiwa ni ishara ya mshikamano na umoja uliopo kati yao washirika waosali katika la TGRC Mazimbu Barakuda Morogoro.

Aidha amesema ameomba waombaji popote walipo nchini Tanzania na nje ya Nchi, kuendelea kumwombea na kuombea uzinduzi wake ili ufanikiwe zaidi kama anavyokusudia moyoni mwake.

Albamu ya Antonia Emmanuel ina jumla ya nyimbo nane (8) ambayo itazinduliwa tarehe 24/7/2022 saa 8 Mchana katika Kanisa la TRGC, kanisa linalochungwa na Mchungaji Jailos Maloda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news