Uhamiaji imarisheni usalama mipakani asema Waziri Masauni

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Yusufu Masauni ameitaka Idara ya Uhamiaji nchini kusimamia uingiaji na utokaji wa wageni katika mipaka ya nchi kwa kufuata sheria za nchi.
Waziri Masauni ameyasema hayo Juni 15,2022 Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha alipofika kukagua maendeleo ya Zoezi la Uwekaji wa Alama za Mipaka katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.

Aidha, Masauni amebainisha kuwa serikali itafanya uhakiki wa kina kubaini uendeshaji wa Asasi za Kiraia nchini kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na zile zitakazokiuka zitachukuliwa hatua kali za kisheria.

Masauni ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya zoezi na kuwataka wahusika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, alimueleza Mhe. Masauni kuwa amepokea maelekezo yake na kwamba atahakikisha kuwa hali ya usalama wa wananchi na mali zao inaendelea kuimarishwa wilayani Ngorongoro na kuwa zoezi hilo litaendelea kwa hali ya amani na utulivu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news