Balozi Polepole ateta na Balozi wa Zimbabwe nchini Malawi

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Tanzania nchini Malawi,Humphrey Polepole amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Zimbambwe nchini Malawi na Amidi wa Mabalozi wa Nchi za Afrika, Dkt. Nancy Saungweme.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Jumatatu Juni 20, 2022 Balozi Polepole ametumia nafasi hiyo kumhakikishia ushirikiano katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kidiplomasia baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nchi ya Zimbabwe.

Kwa upande wake Balozi Dkt. Saungweme amesema kuwa kuwa, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mojawapo ya nchi marafiki wa Zimbambwe tangu harakati za ukombozi hata sasa.

Pia ametumia nafasi hiyo kuishukuru Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kupigania haki za Wazimbabwe na kwa umahususi katika kampeni ya kuiondolea vikwazo vya kiuchumi mara moja nchi.

Post a Comment

0 Comments