CCWT:Sensa ya Watu na Makazi ni muhimu sana kwa wafugaji, tupo tayari kuhesabiwa

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Jeremiah Wambura anaendelea na ziara yake katika mikoa yote Tanzania Bara ambapo Juni 2, 2022 alizuru katika Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuzungunza na wafugaji Wilaya ya Chunya.
Wambura amesema, lengo kubwa ni kuhakikisha wafugaji wanashiriki vyema kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23, 2022, kujiandaa kuhesabiwa pamoja na zoezi la utambuzi wa mifugo lakini pia kufanya usajili wa mifugo ya wafugaji.

“Ninazisisitiza halmashauri zote ambazo hazijafanya hivyo kuanza mara moja kwani ukomo wa usajili wa mifugo kwa hihari ni Agosti 31, mwaka huu lakini pia Sensa ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa,”amesema Mwenyekiti Wambura.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa, ameamua kufanya ziara hiyo ili kuwahamasisha wafugaji kushiriki vyema, lakini pia kuwakumbusha kuwa hitimisho lake ni Agosti 23, 2022.

“Nikiwa mwenyekiti wa wafugaji Tanzania ni wajibu wangu kuwakumbusha wafugaji mambo muhimu wanayotakiwa kuyafanya kwa ajili ya maendeleo yao na mifugo yao,” amesema Mwenyekiti Wambura na kuongeza ;
“Sio wote wenye uelewa kuhusiana na mambo haya na ndio maana nimeamua kufanya ziara kwa ajili ya kutoa elimu ili waweze kuelewa na kuwa tayari kwa ajili ya kutoa ushirikiano,”amesema Mwenyekiti Wambura.

Mwenyekiti kwenye ziara yake aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ukaguzi na Haki za Wanyama kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Annete Kitambi, Mratibu wa Sekta ya Mifugo kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI Dkt. Bertha Dugange.

Aidha, Dkt.Annete alieleza sifa za utambuzi na kusisitiza wafugaji kuekeza kwenye ujenzi wa miundombinu na upandaji wa malisho.

Naye Mratibu wa Sekta ya Mifugo kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt.Bertha Dugange amesistiza juu ya ushirikiano wa wadau katika mnyororo wa thamani wa Sekta ya Mifugo na kuhamasisha wafugaji kuchangamkia fursa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news