DC ataka utunzaji vyanzo vya maji wilayani Geita

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Geita mkoani Geita,Mhe.Wilson Shimo amezitaka Jumuiya za Watoa Huduma za Maji ngazi ya Jamii (CBWSO’s) kuongeza weledi katika utunzaji wa vyanzo vya maji ili viweze kuwa endelevu na salama kwa watumiaji.
Mhe. Shimo amesema hayo katika mkutano mkuu wa CBWSO’s wilayani Geita kilichofanyika katika ukumbi wa Alphendo amesema jumuiya hizo zinapaswa kutunza vyanzo vya maji katika maeneo yao.

Amesema,  suala la kutunza vyanzo vya maji ni jukumu la kila mmoja hasa jumuiya za watoa huduma za maji ngazi ya jamii ili kutoa maji safi na salama kwa wananchi.
Amewata kupanda miti ambayo ni rafiki na maji katika vyanzo vya maji ili kuweza kuvitunza pamoja na kulinda vyanzo hivyo ili wananchi wa maeneo husika waweze kupata maji safi na salama.

Hata hivyo,  Shimo ameipongeza RUWASA Wilaya ya Geita kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza vyema miradi mbalimbali ya maji ndani ya halmashauri ya wilaya ya Geita.
Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Geita, Sande Batakanwa amemuhakikishia Mhe. Wilson Shimo kuwa atahikisha anasimamia vyema Jumuiya za watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO) ili ziweze kusimamia vyema vyanzo vya maji.

Sande amesema,  atasimamia kikamilifu zoezi la upandaji miti rafiki katika vyanzo vya maji kama alivyoagiza mhe, mkuu wa wilaya kwa lengo la kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa pamoja na kutunzwa ili viweze kutoa maji kwa mda mrefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news