DC Msafiri aonya matumizi ya bunduki, silaha za jadi

NA DIRAMAKINI

WAFUGAJI wanaotumia vibaya bunduki na silaha za jadi wilayani Kibaha watachukuliwa hatua kali za kisheria endapo wataendelea na vitendo vya kuwatishia na kuwapiga wakulima kwa kutumia silaha hizo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Sara Msafiri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Wilaya ametoa maagizo hayo kwenye Kijiji cha Kitomondo Kata ya Ruvu na kupata taarifa juu ya baadhi ya wafugaji wavamizi wanaotishia na kuwapiga wakulima kwa silaha mbalimbali na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.

Msafiri amesema kuwa, baadhi ya wafugaji hao wamekuwa na matumizi mabaya ya silaha mbalimbali zikiwemo bunduki na zile za jadi kama mishale na upinde na kutaka kukomeshwa kwa tabia hiyo na endapo kutatokea tukio la aina hiyo kamati hiyo haitosita kukomesha matumizi ya silaha hizo.

Katika hatua nyingine amepiga marufuku mifugo kusambaza kiholela na kuagiza Serikali ya kijiji cha Kitomondo kukutana na wafugaji wiki ijayo ili kubaini wafugaji wavamizi na idadi ya wafugaji wanaotambuliwa kuomba kibali halali kwenye mkutano wa Kijiji.

Baadhi ya wakulima wa Kitomondo wamesema kuwa kumezuka wimbi la mifugo na wafugaji wavamizi Hali inayosababisha kuliwa mazao Yao na kupata hasara.

Ofisa mifugo kata ya Ruvu Francis Ekoni amepokea maagizo hayo na kusema wafugaji wanaotambulika katika kijiji cha Kitomondo ni wanne tu.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibaha, Ombeni Msangi ameeleza kuwa, kuingiza mifugo eneo jingine na kijiji kingine kwa wakulima ni kosa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news