Dkt.Jingu aongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi 2022

NA MWANDISHI WETU

KAMATI ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi imefanya kikao kazi cha utekelezaji wa Sensa ya Mwaka 2022. Katika kikao hiki, Kamati imepokea taarifa ya hali ya maandalizi kuelekea Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 itakayofanyika tarehe 23 Agosti, 2022.
Kikao cha Tano Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kikiendelea Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Juni, 2022.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Thabit Idarous Faina akizungumza jambo wakati wa kikao cha Tano cha Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msingwa akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia kikao.

Jukumu kubwa la Kamati ya Ushauri ni kuishauri Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa inayoongozwa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar namna bora ya utekelezaji wa Sensa.

Aidha kikao kilifanyika tarehe 04 Juni, 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Mhe. Anne Makinda akichangia na kufafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu Mifugo Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao hicho
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe akizungumza jambo wakati wa kikao hicho, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akifuatiwa na Katibu Mkuu Mifugo Bw. Tixon Nzunda pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro.
Sehemu ya wajumbe wa kikao wakifuatilia kikao hicho.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akiongoza kikao cha Tano cha Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam tarehe 4 Juni, 2022.

Kaulimbiu ya Sesa ya Watu na Makazi 2022 ni “Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa”.

Post a Comment

0 Comments