EALA lawapongeza na kuwaenzi Hayati Kibaki,Jacob Oulanyah

NA DIRAMAKINI 

BUNGE la Afrika Mashariki limewapongeza na kuwaenzi hayati Spika mstaafu wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah na Hayati Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki kwa kudumisha demokrasia na utawala bora.
Kwa nyakati toafauti waheshimiwa wabunge, Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, Bi. Akol Rose Okullu,Dkt. Rwigema Pierre Celestin na James Kakooza walibainisha kuwa, viongozi hao wana mchango mkubwa katika bunge na jumuiya hiyo, hivyo wataendelewa kuenziwa nyakati zote kwa ustawi bora wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Naye Mheshimiwa Fatuma Ndangiza amesema kwamba, ipo haja kwa Bunge hilo kuandaa mswada wa kupitisha sheria ya kuwaenzi viongozi waliotangulia mbele za haki ili kuendelea kuwaenzi viongozi na kujenga utamaduni huo.

Mheshimiwa Ndangiza amesema kuwa, ukiangalia nchi ya Kenya imekuwa ikisifika kwa katiba bora,kwa msingi huo utaona mchango mkubwa uliotolewa na Hayati Mwai Kibaki kujenga demokrasia wakati wa uongozi wake. 

Amesema, viongozi hao ni wa kuigwa kwa mema yao yote na kuendelezwa na Bunge hilo kwa kuendelea kuwaenzi na kukumbuka mchango wao kwa Taifa lao na mataifa ndani ya jumuiya.

"Mwai Kibaki alianzisha Katiba na kutoa mchango mkubwa ili nchi iwe na katiba nzuri sasa hivi miongoni mwa katiba ya viwango ni ya Kenya hii inasaidia nchi kuwa na amani,"amesema Ndangiza.

Pia amesema, Bunge hilo linapaswa kuendelea kujenga utamaduni huo endelevu wa kukumbuka viongozi kwa wabunge kuleta muswada ili uingie kwenye sheria za jumuiya.

Mheshimiwa Ndangiza amesema kuwa, hayati Spika Jacob alisaidia kuimarika kwa demokrasia nchini Rwanda na ,alitoa mchango kwa jamii kuwasaidia wenye maisha ya chini na yatima na kuendeleza demokrasia ambayo ikiigwa na vijana itawasaidia.

Hata hivyo,wawakilishi hao wa Afrika Mashariki walipongeza na kuonyesha utayari wa kuendelea kuwaenzi viongozi mbalimbali wakiwemo Hayati Mwai Kibaki na Spika Jacob Oulanyah.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news